Swali: 4- Soma Suratu Qari'a na uitafsiri.

Jawabu: Suratul Qaari'a na tafsiri yake:

Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.

"Kiyama chenye kugonga nyoyo za watu" "Ni nini kinachogonga" "Ni kipi kinachokujuza ni kipi kinachogonga?" "Siku hiyo watu watakuwa , kwa wingi wao, kugawanyika kwao na kuzunguka kwao, ni kama panzi walioenea. Nao ni wale wanaojitupa motoni." "Na majabali yatakuwa ni kama pamba yenye rangi tofauti inayochambuliwa kwa mkono ikawa ni mapepe na ikamalizika." "Basi mwenye kuwa mizani ya mema yake ni nzito," "atakuwa kwenye maisha ya kuridhika Peponi." "Ama mwenye kuwa mizani ya mema yake ni nyepesi na mizani ya maovu yake ni nzito" "Basi makazi yake yatakuwa ni moto wa Hawiya" "Ni kipi kinachokujuza ni upi moto wa Hawiya?" "Ni moto mkali" [Suratul Qaria: 1-11]

Tafsiri:

"Kiyama kigongacho" Kiyama kinachogonga nyoyo za watu kwa ukubwa wa vitisho vyake.

"Ni nini kigongacho" Ni muda gani huu ambao utagonga nyoyo za watu kwa ukubwa wa vitisho vyake?!

"Na nini kitakachokujulisha ni kipi kigongacho?" Ni kipi kilichokufahamisha ewe Mtume ni saa gani hii ambayo inagonga nyoyo za watu kwa ukubwa wa vitisho vyake?! Hiyo ni siku ya kiyama.

"Siku hiyo watu watakuwa , kwa wingi wao, kugawanyika kwao na kuzunguka kwao, ni kama panzi walioenea. Nao ni wale wanaojitupa motoni." Siku ambayo itagonga nyoyo za watu watakuwa mfano wa panzi waliotawanyika wanaozagaa huku na kule.

"Na milima itakuwa kama sufi iliyotawanywa" Na itakuwa milima mfano wa sufi iliyochambuliwa kulingana na wepesi wa kupeperuka kwake na kutembea kwake.

"Ama itakayekuwa mizito mizani yake": Ama ambaye matendo yake mema yatazidi matendo yake mabaya.

"Basi huyo atakuwa katika maisha ya kuridhika": Yaani atakuwa katika maisha ya kuridhika atakayoyapata peponi.

"Ama itakayekuwa mwepesi mizani yake": Ama ambaye matendo yake maovu yatazidi matendo yake mema.

"Basi makazi yake ni moto wa Hawiya" Yaani: Maskani yake na makazi yake siku ya kiyama ni Jahanamu.

"Ni nini kitakachokujulisha ni ipi hiyo Hawiya": Ni kipi kitakachokufahamisha ewe Mtume ni ipi hiyo?!

"Ni moto mkali": Nao ni moto wenye joto kali.